Kartra

Mdogo wa Mbappé Asaini PSG

MDOGO wa nyota wa kabumbu wa Klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappé aitwaye Ethan Mbappe mwenye umri wa miaka 15, amesaini kandarasi mpya ya miaka mitatu hadi 2024 klabu hiyo ya Paris Saint-Germain.

 

Ethan ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati au winga ambaye alikuwa na kiwango bora kabisa kwenye mashindano ya International Champions Cup ya mwaka 2019.

 

Pia PSG kupitia tovuti yake wametangaza kumsajili Kinda Senny Mayulu ambaye amezaliwa mwaka 2006 na amesaini mkataba wa miaka mitatu mpaka 2024.


Toa comment