The House of Favourite Newspapers

Mdogo wa Ngoma Agongwa, Afariki Dunia

0

donald-ngoma-yanga_mqjc36fbxrqu1k9l2138qyhm3Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.

Wilbert Molandi na Said Ally
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Donald Ngoma anatarajiwa kuukosa mchezo wa kimataifa kesho Jumamosi wakati timu yake itakapopambana na Cercle de Joachim ya Mouritius kwenye Uwanja wa Taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Cercle de Joachim baada ya awali kupata ushindi wa bao 1-0 nchini Mouritius, ambapo mfungaji alikuwa ni Ngoma.

Ngoma-3.jpg Kocha Pluijm (kulia) akisalimiana na Ngoma.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema Ngoma amefiwa na mdogo wake, taarifa ambazo alizipata juzi Jumatano mara baada ya mechi dhidi ya JKT Mlale kwenye Uwanja wa Taifa na aliondoka alfajiri ya jana kuelekea msibani.
“Amefiwa na mdogo wake wa baba mmoja ambaye alikuwa kama mwanaye, Ngoma ndiye aliyekuwa akimlea, ameondoka leo (jana) alfajiri,” alisema Muro na kuongeza:
“Mdogo wake alifariki uwanjani wakati anatolewa kwa ajili ya kupelekwa hospitali, aligongana na mwenzake wakati wa kuwania mpira.

DSC_6724Mashabiki wa Yanga wakifanya yao.

“Tumempatia muda wa mapumziko wa wiki moja kisha akimaliza arejee nchini ambapo anatarajiwa kurejea kabla ya mechi dhidi ya Azam (Machi 5, 2016).”Aidha, Muro alisema kambi ya Yanga ipo kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kesho, ambapo pia watawakosa Haruna Niyonzima na Salum Telela ambao ni majeruhi huku akisema kiingilio cha chini katika mchezo wa kesho kitakuwa shilingi 5,000.
Wakati huohuo, kikosi cha Cercle de Joachim kiliwasili jijini Dar es Salaam, jana saa 12 jioni. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kocha wa timu hiyo, Abdel Ben Kacem alisema:
“Tumekuja na wachezaji 21 na viongozi sita, tupo kamili na tunajua kuwa Yanga wameshinda mechi yao ya juzi. Tuna matumaini makubwa ya kupata ushindi, sisi kuwa ugenini siyo tatizo.”

Leave A Reply