The House of Favourite Newspapers

MDUDE CHADEMA AFUNGUKA ‘ALIVYOTEKWA’ – VIDEO

BAADA kupatikana akiwa hai baada ya kutupwa katika Kijiji cha Makwenje, kata ya Inyala mkoani Mbeya, mfanyabiashara na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali ‘Mdude Chadema’, aliyedaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana amefunguka kuhusu kilichotokea.

 

Mdude alizungumza na vyombo vya habari jana, Alhamisi akiwa kitandani baada ya kupatikana na kusema alishauriwa aongee badae akipata nafuu lakini akasema yeye sio kama watu wengine ambao alidai wakitekwa wanakaa kimya hawasemi ukweli. Amesema hajui ‘watekaji’ walimfanya nini anaweza kufa hajasema ukweli.

 

Mdude anadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake Vwawa, Mbozi mkoani Songwe mwishoni mwa wiki jana.

 

MSIKIE MDUDE CHADEMA AKIFUNGUKA

Comments are closed.