Mechi ya Simba: Championi, Spoti Xtra Yawalipia Tiketi Wasomaji Wake

 

TIMU ya Masoko ya Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra jana Jumatano, Januari 7, 2021, ilitinga katika viunga vya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na kugawa kwa wasomaji wake tiketi za kutazama kuingia mechi kwenye mchuano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Simba SC na FC Platinum ya Zimbabwe.

 

 

 

Hii imekuwa kawaida ya Kampuni ya Global Publishers kurudisha fadhila kwa wasomaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali na kuendelea kufanya promosheni ya magazeti yake ya Championi na Spoti Xtra yanayoongoza kwa kusomwa nchini.

 

 

“Hii imekuwa desturi kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono sana, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kwa kuwapa kile tunachokipata kutoka kwao, ili wajisikie kama familia ya Championi na Spoti Xtra,” alisema Anthony Adam ambaye ni Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers wakati wakigawa tiketi hizo kwa mashabiki.

 

 

Katika mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Simba iliibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya FC Platinum na kuifanya Simba kusonga mbele katika hatua ya makundi.

 

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)Tecno


Toa comment