The House of Favourite Newspapers

Mechi ya Yanga na Azam yahamishwa

SHIRIKISHO la Soka la Tanzania(TFF) limeziambia Yanga na Azam kwamba wasahau kucheza kwenye kapeti nyasi za Taifa Jumatatu jioni. Mechi hiyo ni muhimu kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwani Yanga inaongoza msimamo huku Azam ikiwania kwenda kileleni.

 

Dakika chache kabla ya kuanza mechi ya Manchester United na Man City usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Mratibu wa Azam Fc, Philip Alando aliithibitishia Spoti Xtra kwamba uwanja umebadilishwa na sasa kipute kitapigwa Uhuru kwenye nyasi bandia.

Uhuru ambao umepakana na Taifa unabeba mashabiki 23,000. Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera mwenye taaluma ya ualimu wa sekondari, alisema kwamba wameambiwa uwanja hauko vizuri.

 

“TFF wametuambia kwamba Uwanja wa Taifa umetumika sana, kwahiyo unahitaji kupumzishwa na kuwekwa sawa kwa hiyo mechi yetu itabidi tucheze Uhuru kwenye nyasi bandia,”alisema Alando ambaye majeraha ya mara kwa mara yalimlazimisha kustaafu soka akicheza kama straika.

 

Kiongozi huyo msomi na msomaji mzuri wa Spoti Xtra alisisitiza jana kwamba hawatishwi na mabadiliko ya uwanja kwani wamejiandaa kupambana kwenye mazingira yoyote

Comments are closed.