The House of Favourite Newspapers

Mechi ya Yanga na Mbao Yahamishwa Uwanja

0

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limethibitisha kuhamishwa kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ hatua ya 32 kati ya Young Africans dhidi ya Mbao FC kutoka Dar es salaam na kuupeleka jijini Mwanza.

Awali mchezo huo ambao Young Africans ni mwenyeji ulikua umepangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumamosi (Januari 29), na sasa utapigwa jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba siku hiyo.

Taarifa kutoka TFF iliyosainiwa na Salum Madadi kwa niaba ya Katibu Mkuu, imeeleza kuwa Young Africans imeombwa mchezo huo uchezwe jijini Mwanza kufuatia uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika kwa matumizi mengine siku ya Jumamosi (Januari 29).

Maamuzi hayo yataifanya Yanga SC kucheza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/22, baada ya Wapinzani wao wa Jadi Simba SC kuepelekwa kwenye Uwanja huo na Ruvu Shooting kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Leave A Reply