visa

Meddie Kagere aendelea kutikisa CAF

Meddie Kagere katikati akifanya yake.

STRAIKA wa Simba, Mnyar-wanda, Meddie Kagere bado anaendelea kushirikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati licha ya timu yake kuondolewa.

 

Hii ni rekodi ambayo nyota huyo wa Simba ameweka katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo timu hiyo ilitolewa katika hatua robo fainali ya michuano hiyo.

 

Kagere katika orodha ya wafungaji bora anashika nafasi ya pili akiwa na mabao sita huku kinara akiwa na mabao saba ambaye ni Moataz Al Mehdi wa Al Nasr ambaye yeye timu yake ilitolewa hatua za awali kabisa kwenye michuano hiyo.

Kwa upande wa wafungaji hao wa Caf mpaka sasa kwa timu ambazo zimetinga fainali, mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ni matano ni Mohammed Nahir wa Wydad sawa na Clatous Chama wa Simba.

Nahir ambaye atacheza fainali na Esperance ndiye mwenye nafasi ya kuvunja rekodi ya ufungaji kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Toa comment