The House of Favourite Newspapers

Meek Mill, Jay-Z Waanzisha Taasisi Kusaidia Wafungwa

 

MARAPA wawili wa Hip Hop wa Marekani, Jay Z na Meek Mill,  wameanzisha taasisi ya kutoa msaada wa kisheria inayojulikana kwa jina la ‘Reform’ kwa Wamarekani weusi waliofungwa jela nchini Marekani,  ambayo itakuwa inasimamiwa na kuongozwa na Van Jones mtangazaji wa shirika la habari la CNN.

 

Van Jones

 

Reform ina mpango wa kutoa msaada wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 50 (Tsh bilioni 115.8)

 

Meek Mill alifunguka na kusema, “Ni jambo  muhimu sana ambalo sijawahi kulifanya kwenye maisha yangu kwa watu ambao hawana sauti, kama ulifikiri kesi yangu haikunistahili, basi kuna mamilioni ya watu wanateseka kwa kukamatwa na uhalifu ambao hawakushiriki.”

 

 

Meek aliendelea kwa kusema, “Kwa muungano huu tunataka kubadilisha sheria ambazo tarehe zake zimepitwa na wakati ili kuwapa watu tumaini.”

Naye Jay Z alisema taasisi hiyo hailengi kuwasaidia wanaotenda makosa lakini inalenga kuwasaidia wale ambao wamekamatwa kwa makosa wasiyoyafanya.

 

 

“Nataka tueleweke vyema, kama mtu amefanya makosa anapaswa kwenda jela kwa makosa yake lakini mambo haya hayana usawa na dunia nzima inajua hivyo,” alisema.

 

 

Kwa mujibu wa kundi la harakati za haki za binadamu la NAACP wastani wa Wamarekani weusi watano hufungwa jela ikilinganishwa na Mmarekani mweupe mmoja.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.