The House of Favourite Newspapers

Meek Mill na Drake wamaliza bifu lao rasmi

0

New York, Marekani

WAKALI wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Robert Williams ‘Meek Mill’ na Aubrey Graham ‘Drake’ waliokuwa kwenye bifu kali kiasi cha kupigana vijembe kwenye mashairi, mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na kwenye matamasha yao limekwisha rasmi.

Wakali wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Robert Williams ‘Meek Mill’ na Aubrey Graham ‘Drake’ wakishikana mikono.

Meek  ndiye alikuwa wa kwanza kusalimu amri baada ya hivi karibuni ‘kumfolow’ Drake kwenye ukurasa wake wa Instagram huku pia akimpongeza kwa Kanda Mseto yake mpya anayotarajia kuiachia siku za hivi karibuni akimshirikisha rapa Future.

Bifu la wawili hao lilianza mapema mwaka huu baada ya Meek ‘kumdiss’ Drake kuwa hana uwezo wa kujilinganisha naye kutokana na tetesi zilizokuwa zimeenea za msanii huyo kuandikiwa mashairi  kwenye nyimbo zake nyingi na mwandishi wa mashairi maarufu Marekani, Quentin Miller likaendelea na kushika kasi Drake alipomrudishia mashambulizi Meek kwenye wimbo wake wa michano huru wa Back to Back.

Leave A Reply