The House of Favourite Newspapers

Meghan Markle Ahudhuria Mashindano ya Kwanza ya Farasi

WANANDOA Meghan Markle na mwanamfalme wa Uingereza, Prince Harry,  amehudhuria kwa mara ya kwanza mashindano ya farasi maalum kwa familia ya kifalme yanayofanyika kwa siku tano ambayo yanajulikana kama Ascot Racecourse, ambayo ni moja ya matukio makubwa zaidi nchini Uingereza.

Meghan na Prince Harry.

Wawili hao ambao kwa majina ya kifalme wanajulikana kama ‘Duke and Duchess of Sussex’, waliingia katika viwanja hivyo wakiwa katika gari maalum lenye kukokotwa na farasi ambapo waliungana na Malkia Elizabeth, Prince Edward na Sophie, ‘Countess of Wessex’.

Wanandoa hao mbali na kufurahia mapochopocho mbalimbali eneo hilo, walikuwa pia wamevaa mavazi yanayoendana na tukio hilo ambapo wanawake huvaa magauni mang’avu na kofia maalum, na wanaume huvaa nguo za kitamaduni za kutokea nyakati za asubuhi na kofia.

attend

Comments are closed.