The House of Favourite Newspapers

Meja Kunta Afiwa na mama yake mzazi, Kuzikwa Kesho Yombo Dovya

Msanii maarufu wa muziki wa Singeli nchini, Meja Kunta, amepata pigo baada ya kuondokewa na mama yake mzazi, Mosi Mkalawile.

Global TV imefika nyumbani kwao, Mtaa wa Maputo, Temeke jijini Dar es Salaam ambako ndiko msiba ulipo.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho, April 14, 2025 katika Makaburi ya Yombo Dovya.