Meli 2 Zenye Bendera ya Tanzania Zawaka Moto Urusi, 14 Wafariki

 

WATU 14 wanadaiwa kupoteza maisha na wengine watano hawajulikani walipo kufuatia meli mbili za mizigo Maestro na Candy, zilizokuwa zikipeperusha bendera ya Tanzania zimewaka moto  kando ya pwani ya Crimea kwenye Bahari Nyeusi nchini Urusi.

 

Kwa mujibu wa Wizara ya Usafirishaji ya Urusi, meli hizo zilikuwa na jumla ya watu 31 ambapo 16 ni Waturuki na 15 ni Wahindi na kwamba zimeteketea baada kutokea mlipuko mkubwa wakati wa kuhamisha mafuta kutoka kwnye tenki moja kwenda jingine.

 

Taarifa zinasema tukio hilo limetokea karibu na Mlango Bahari wa Kerch ambako pana msuguano mkubwa baina ya Russia na Ukraine,  na katika siku za karibuni Russia ilitaifisha meli tatu za Ukraine zilizokuwa zikijaribu kupita sehemu hiyo.

 

Wanamaji wa Russia walijaribu kuwaokoa mabaharia wa meli hizo ambao walijirusha baharini ili kuokoa maisha hao.

 

Kikosi cha uokoaji nchini Urusi kimesema watu 12 wameokolewa wakiwa hai ambapo miili 11 ya  ikiopolewa na miili mitatu bado haijapatikana.

 

CHANZO: INDEPENDENT


Loading...

Toa comment