The House of Favourite Newspapers

Meli Kubwa Ya Mafuta Yatekwa Somalia Huku Wamarekani Wakishuhudia

Meli za kupambana na maharamia za Marekani.

Meli kubwa iliyokuwa na shehena kubwa ya mafuta, iliyokuwa ikitokea Djibout kwenda Mogadishu, Somalia imetekwa na maharamia wa Kisomali, kwenye ufukwe wa Somalia, jirani na meli kubwa ya kivita ya Marekani iitwayo U.S. Navy’s 5th Fleet.

Duru za kiusalama zinasema, mahali meli hiyo ilipotekwa, panaonekana vizuri na rada za meli hiyo ya kivita ya Marekani inayoongozwa na mitambo iliyopo nchin Bahrain, jambo linaloashiria kwamba huenda Wamarekani walishuhudia mchezo mzima lakini wakazidiwa akili na watekaji.

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda, boti mbili ziendazo kasi zilionekana zikiifuata meli hiyo kwa kasi, jambo lililomfanya nahodha kubadili mwelekeo lakini muda mfupi baadaye, tayari boti hizo zilizokuwa na watu waliojihami kwa silaha nzito, zilikuwa zimeifikia na kufanikiwa kuiteka.

Kwa mujibu wa msemaji wa taasisi ya kupambana na maharamia ya Oceans Beyond Piracy, John Steed, ndani ya meli hiyo kulikuwa na watu zaidi ya 12 na hilo linatajwa kuwa tukio kubwa zaidi la utekaji tangu mwaka 2012, na kwamba huenda ni salamu za magaidi kwa Rais Donald Trump wa Marekani baada ya kuingia madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia zilizothibitishwa na maafisa wa Marekani, watekaji wanadai kiwango kikubwa cha fedha ili waiachie meli hiyo na kwamba uchunguzi zaidi na mazungumzo na watekaji, zinaendelea.

Meli hiyo inashukiwa kuwa huenda ni ya kutoka Falme za Kiarabu, Sri Lanka, Ugiriki au Comoro na kwamba juhudi za kuitambua asili yake, zimekuwa ngumu kwani watekaji walitoa bendera zote baada ya kuiteka.

Comments are closed.