The House of Favourite Newspapers

Melissa Aibuka Mshindi Airtel Trace Music, Azowa Milion 50

0

1

2       Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza akimkabidhi mshindi wa kwanza wa Airtel Trace Star, Melissa John hundi ya mfano yenye thamani ya sh.50 milioni.
3. Mshindi wa pili,Nandy Charles (mwenye ngu ya bluu) akiwa na mfano wa hundi ya milioni tano.Mshindi wa pili, Nandy Charles (mwenye nguo ya bluu) akiwa ameshikilia hundi ya shilingi milioni tano.
4.Majaji wa shindano hilo wakifuatilia burudani iliyokuwa ikitolewa na washiriki hao.Majaji wa shindano hilo wakifuatilia burudani iliyokuwa ikitolewa na washiriki hao.
5.Melissa akifanya mahojiano na wanahabari.Melissa akifanya mahojiano na wanahabari.
6.Sehemu ya wageni waalikwa waliokuwa wamefika kwenye hafla hiyo.Sehemu ya wageni waaliwa waliokuwa wamefika kwenye hafla hiyo.
7.Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia hafla hiyo.Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia hafla hiyo.
8Mshindi wa tatu, Salim Mlindima akifanya mahojiano na wanahabari.
9.Washiriki wa shindano hilo wakipata maelekezo kutoka kwa MC wa hafala hiyo.Washiriki wa shindano hilo wakipata maelekezo kutoka kwa MC wa hafla hiyo.
10.Melissa akitoa burudani mara baada ya kuibuka mshindiMelissa akitoa burudani mara baada kuibuka mshindi.

KAMPUNI ya Simu ya Mkononi ya Airtel usiku wa kuamkia leo imemtangaza rasmi mshindi wa Shindano la Airtel Trace Music Star, Melissa John baada ya kuwabwaga washiriki wengine waliokuwa wameingia tano bora na kujizolea kitita cha shilingi milioni hamsini.

Miongoni mwa washiriki watano walioingia tatu bora ni Melissa John, aliyepewa hundi ya shilingi milioni hamsini, Nandy Charles aliyepewa naye hundi ya shilingi milioni tano, Salim Mlindila hundi ya shilingi milioni mbili.

Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi uliopo Jengo la Kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, lilikuwa na lengo la kusaka na kukuza vipaji vya muziki na kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa Kitanzania na Afrika kujulikana katika anga za muziki duniani.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya shindano hilo kuisha Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema kuwa wanayo furaha kubwa kumtangaza mshindi wa shindano hilo kwa kuwa majaji walifanya kazi yao kubwa ya kuona nani anafaa zaidi kutoka kwenye washiriki watano ambao waliingia fainali.

“Nawapongeza sana washiriki wote watano waliokuwa wameingia tano bora kwani wote ni washindi lakini aliyetakiwa kuwawakilisha ni mmoja tu hivyo niwatie moyo wasikate tamaa, washiriki hao tuliwapata kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimaye majaji walisikiliza vipaji vyao na sasa ndiyo mshindi amepatikana,” alisema Matinde.

Aidha aliongeza kuwa mshindi huyo atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Star ya Afrika nchini Nigeria yatakayoshirikisha nchi mbalimbali barani Afrika na katika mashindano hayo mshindi atakayepatikana atarekodiwa nyimbo zake na wasanii wakubwa nchini Marekani.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply