Meneja Aingilia Penzi la Ebitoke, Mlela

MENEJA wa zamani wa mchekeshaji Ebitoke, Bhoke Rioba ameingilia kati suala la msanii wake huyo kuanika uhusiano wake na mwigizaji Yusuf Mlela. 

 

Meneja huyo amemtahadharisha Ebitoke kuwa asitegemee kupata dili zozote kama anashinda mitandaoni kuanika mapenzi yake na wanaume.

 

“Uhusiano na maisha ambayo anaishi Ebitoke siyakubali kwa sababu huwezi kupata dili ukiwa unamuonesha mwanaume kila siku kwenye mitandao ya kijamii au ukiposti picha unatukanwa matusi. Ndiyo maana hata kuna kipindi aliposti picha akiwa amevaa nguo za ufukweni nikazifuta,” amsema Bhoke.

Uhusiano wa Ebitoke na Mlela unatajwa kuwa ndiyo mpya mjini kwa sasa ambapo walionekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja na kuposti picha katika mitandao ya kijamii.

 

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Ebitoke aliandika; “Hivi binadamu mkoje jamani? Ina maana mimi siyo mwanamke mpaka mnitoe kasoro kiasi hiki? Mimi siwezi kupendwa? Acheni wivu, watu wakipendana ni makosa? Haya nipumzisheni leo ndiyo mwanzo na mwisho kumposti, mengine private kaah


Loading...

Toa comment