The House of Favourite Newspapers

MENEJA WA NYANZA AFUNGWA MIAKA 20

0

ALIYEKUWA meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater,  leo amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwenda jela  miaka 20 baada ya kukutwa na kucha 17 za  simba.

 

Mtuhumiwa huyo amehukumiwa kwenda jela kulipa faini ya Shilingi milioni 534.

 

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha, ambapo amesema amesikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashtaka na vielelezo vitatu na utetezi wa mshtakiwa mwenyewe alioutoa.

 

Mkeha alisema Mahakama imemkuta mtuhumiwa akiwa na hatia  baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi hiyo pasipo shaka na kueleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa ndani ya mahakama hiyo vilikuwa  ni kucha za simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.

 

Mtuhumiwa huyo alishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani.

 

 

Leave A Reply