The House of Favourite Newspapers

Meneja wa TRA Aliyekataa Mabilioni Akapongezwa na JPM Huyu Hapa! – VIDEO

Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutambua juhudi zake za kupinga rushwa baada ya kukataa kupokea rushwa.

Akizungumza na Global TV manager huyo amesema kitendo kilichofanywa na rais mbele ya viongozi wenzake na umma wa watanzania kumtambua kwa kitendo alichokifanya ni ishara kuwa alikua sahihi katika maamuzi yake.

Mbibo amebainisha kuwa kila anapokutana na wafanyakazi katika vikao vya ndani vya ofisi lazima wagusie suala la rushwa kwani wanaamini ndio njia sahihi ya kukumbushana na kusisitiza utumishi usiotegemea rushwa.

Hata hivyo Mbibo amewataka baadhi ya wafanyabiashara kuacha tabia ya kujitokeza na kudanganya katika zoezi la kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo vilivyotolewa na Rais Magufuli ili wavipate jambo ambalo si sawa kwani vitambulisho hivyo vimetolewa kwa kuwalenga wafanyabiashara wadogo wadogo.

Comments are closed.