The House of Favourite Newspapers

MENEJA: WEMA HAKUKATWA UTUMBO

Wema Sepetu

MENEJA wa muigizaji Wema Sepetu, Neema Ndepanya amefungukia madai ya msanii wake kukatwa utumbo nchini India ili kujipunguza mwili kuwa hayana ukweli, ni uzushi tu.

Akizungumza na gazeti hili, Neema alisema habari hizo zilizozagaa mtandaoni si za kweli bali ni za nia ya kumchafua staa huyo kitu ambacho wao wamekipuuzia.

“Unajua kuna habari nyingine unasikia wala kichwa chako hakiwezi kuuma hata kidogo kwa sababu ni za kizushi, Wema alikwenda India kwa matibabu yake binafsi,” alisema Neema.

Wema alikwenda nchini India hivi karibuni na kuzua gumzo baada ya kushindwa kuhudhuria kesi yake ya madawa ya kulevya katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar na ndipo zilipoibuka taarifa kuwa, amekwenda kukatwa utumbo ili kupunguza unene.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Comments are closed.