MENINA AGEUKIA KWENYE FILAMU

 

Meninah Atik

BAADA ya kimya kirefu kwenye anga la muziki Bongo, mwanamuziki aliyeibukia kwenye Shindano la Bongo Star Search (BSS 2012), Meninah Atik amesema ili kukuza kipaji chake cha sanaa ameamua kugeukia kwenye filamu.  Akipiga stori na Za Motomoto, Meninah alisema kwamba ameamua kuingia kwenye filamu ili kukuza kipaji chake kwani kotekote anaweza na ‘soon’ ataonekana kwenye tamthilia moja kali ambayo watu wakiiona wataufahamu upana wake wa sanaa.

“Kuna kitu kizuri sana nitaonesha kwenye uigizaji wa tamthilia, natumaini kila mtu atapenda, kwani nimeamua kugeukia kidogo na huku baada ya kupumzika kidogo muziki,” alisema Meninah.

Stori: Imelda Mtema, Risasi Mchanganyiko


Loading...

Toa comment