The House of Favourite Newspapers

Menina Ahofia Kupigwa Juju Ujauzito Wake

meninaStori: MAYASA MARIWATA | Gazeti la Amani, Toleo la Desemba 22, 2016

MSANII wa muziki Bongo, Menina Abdulkareem amejikuta akiishi kwa kujifichaficha kutokana na kuhofia macho ya watu sababu ya ujauzito alionao akihofia kupigwa juju, jambo linalomnyima amani ya maisha na kushindwa kufanya mambo yake kwa uhuru.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na msanii huyo kilieleza kuwa, mwanadada huyo licha ya kuwa ana mimba kubwa ya kukaribia kujifungua, tatizo kubwa linalomkabili ni kukwepa macho ya watu pamoja na kuwachenga mapaparazi kwa kuhofia kufotolewa tumbo lake.

Kutokana na ishu hiyo juhudi za kumpata Menina ziligonga mwamba na kufanikiwa kuzungumza na kaka yake Atik ambaye ndiye msemaji wake ambaye alifunguka:

“Dah suala la Menina kuanika tumbo lake ni gumu, anahofia husda za watu, si unajua sio watu wote watakupenda na kukuombea mema, hataki kabisa kuonekana.”

Comments are closed.