Meninah Aibu Yake

NI aibu yake! Ndiyo maneno yaliyowatoka wengi baada ya kuona video chafu inayodaiwa ni ya msanii wa Bongo Fleva na U-MC Bongo, Menina Attick ‘Meninah’ kuvuja mitandaoni.

Baada ya video hiyo inayomuonesha Meninah akifanya mambo ya chumbani na mwanaume ambaye amefichwa sura kuwa gumzo, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimtafuta ambapo alisema kuwa amechezewa mchezo mchafu hivyo anamuachia Mungu.

Mwandishi: Habari yako Meninah?

Meninah: Salama tu, naongea na nani mwenzangu?

Mwandishi: Mimi ni mwandishi wa Global Publishers (Gazeti la Ijumaa Wikienda).

Menina: Niambie…

Mwandishi: Kuna video tumetumiwa hapa ofisini kwetu na inasambaa mitandaoni, unaonekana upo kama ulivyozaliwa kitandani na mwanaume mkivunja amri ya sita, kinyume na taratibu za nchi zinavyotaka, una lipi la kuongea?

Meninah: Kwanza siyo video, ni picha tu, watu ‘wamei-screen shot’ na kuanza kuisambaza mitandaoni. Mimi sina la kusema zaidi ya kumwachia Mungu kwa sababu naamini ni watu wachache ambao wameamua kuisambaza hiyo picha ili wanichafue.

Mwandishi: Ohh! Wewe umeona picha, lakini kuna video kabisa inayokuonesha wewe. Sasa ukiwa kama kioo cha jamii umechukua hatua gani?

Meninah: Siwezi kuchukua hatua yoyote ile, ninamuachia Mungu maana naona watu walizamiria tu kuniumiza.

Stori: Memorise Richard


Loading...

Toa comment