The House of Favourite Newspapers

Mercy Johnson arejesha shepu yake baada ya kujifungua

0

imageNyota wa filamu Nigeria, Mercy Johnson.

NYOTA mcheza sinema wa Nigeria, Mercy Johnson amerejea katika shepu yake bomba baada ya kujifungua mtoto wa tatu. Amerejea umbo lake hilo murua bila ya kutumia mkanda wa kubanana kupunguza ukubwa wa tumbo kama wanavyofanya wanawake wengine siku hizi.

Mwigizaji huyo alionekanamitaani akiwa katika umbo la kuvutia baada ya kurejea kuwapeleke wanaye shuleni na kuingia katika duka moja kununua ‘ice cream’ akiwa na rafiki yake.

Kutokana na shepu yake ya kuvutia si rahisi kuamini kwamba mrembo huyo ana watoto watatu na anategemea hata kupata wa nne karibuni.

Leave A Reply