The House of Favourite Newspapers
gunners X

Meridian Bet Yamshika Mkono Mama Anayeteseka na Mtoto

0

 

 

IKIWA ni siku chache baada ya kipindi cha GLOBALJAMII kinachoruka kupitia GLOBAL TV ONLINE kufanya kipindi na mama Zuhura Shabani (32) ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja aliyetelekezwa na mume wake  baada ya mtoto huyo kuwa na ulemavu, amepewa msaada na MERIDIAN BET.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,  Mkuu wa Utawala wa MERIDIAN BET, Cornelius Boenman,  amesema kampuni hiyo imekuwa ikishiriki katika jamii kwa lengo la kuwasaidia wenye uhitaji sambamba na kuipongeza GLOBAL TV kwa kuendesha kipindi hicho.

Naye Meneja Ustawi wa MERIDIAN BET, Amani Maeda, amesema wao kama kampuni wameguswa na matatizo aliyonayo Zuhura Shabani, hivyo wakaamua kumsaidia mtaji wa biashara kiasi cha shilingi 600000 ili kumsaidia yeye na mtoto wake.

Aidha, Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho, ametumia fursa hiyo kuishukuru MERIDIAN BET kwa msaada huo sambamba na kuyataka makampuni mengine kujitoa kusaidia jamii zenye uhitaji.

Kwa upande wake,  Mtangazaji wa Kipindi cha GLOBALJAMII, Anna Mbawala, amesema kipindi hicho kinalenga kuwafikia Watanzania wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata msaada ambapo ametoa wito kwa jamii kujitokeza kushiriki katika kusaidia jamii ya watu wenye changamoto mbalimbali.

Leave A Reply