The House of Favourite Newspapers

Meridianbet Yafika Zahani Kibaha Kutoa Msaada

Mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet leo wameifikia Kibaha inayopatikana mkoa wa Pwani na kuweza kutoa msaada kwenye moja ya Zahanati inayopatikana katika eneo hilo.

Umekua utaratibu wa taasisi hiyo miaka nenda rudi wakirudisha kwenye jamii yao pale ambapo wanaona kuna changamoto zinaikabili jamii ambayo inawazunguka, Leo ilikua zamu ya Zahanati ya Misugusugu ambao walifika hapo na kutoa msaada.

Vifaa ambavyo vimeweza kutolewa leo ni pamoja mashuka, Vyandarua, pamoja na vifaa vingine vya usafi ambavyo kwa namna moja ama nyingine vitaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kwenye Zahanati hiyo.

Suka mkeka wako kwenye mchezo huu mkali wa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na michezo mingine itakayopigwa wikiendi hii. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Kaimu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko kutoka kampuni ya Meridianbet bwana Abubakar Kulindwa alipata wasaa wa kuzungumza baada kutoa msaada huo “Kwanza kabisa nipende kuwashukuru kwa mapokezi mliyotupatia hapa, Lakini pia ninayo furaha kufanya uwakilishi kwa taasisi yangu pendwa kwa kua sehemu hii ya historia ya kutoa msaada katika Zahanati ambao naamini umegusa utagusa miasha ya wengi”

Haikuishia hapo kwani Mganga wa Zahanati ya Misugusugu inayopatikana katika eneo la Kibaha bwana Nickson Matoh aliweza kutoa shukrani kwa ambacho kimefanywa na kampuni ya Meridianbet kuwakumbuka na kutoa msaada katika Zahanati hiyo.