The House of Favourite Newspapers

Meridianbet Yamuinua Mzee Yusuph

0

Meridianbet leo wamefika eneo la Mbagala Kingugi kwenye moja ya familia zenye uhitaji katika eneo hilo na kufanikiwa kutoa msaada ambao umeiinua familia hiyo kwa kiasi chake.

Kwakua umekua utamaduni wa mabingwa hao wa michezo ya kubashiri kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii yao, Haswa kwa watu wenye uhitaji leo walifika kwa mzee Yusuph Mdogwa mwenye ulemavu wa macho na kutoa msaada.

Familia ya mzee Yusuph ambayo ina uhitaji ilipokea ugeni wa Meridianbet ambapo walifika kwake na kumpatia msaada wa mahitaji mbalimbali ya nyumbani kama Mchele, Sukari, Sabuni, na mafuta ambayo yatamsaidia mzee huyo pamoja na familia.

Bashiri michezo mbalimbali ambayo imepewa ODDS BOMBA pale Meridianbet wikiendi hii Bila kusahau kucheza michezo ya Kasino uibuke mshinde wa Mamilioni

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bi Nancy Ingram alipata nafasi ya kuzungumza machache katika tukio hilo “Kwanza kabisa niseme tu nimefurahi sana kuwepo eneo hilo na kukamilisha hili ambalo tumelifanya hapa kwa Mzee wetu kama taasisi tunajivunia kuendelea kurejesha kwenye jamii yetu haswa kwa wenye uhitaji”

Mzee Yusuph Mdogwa alipata nafasi ya kuzungumza na kutoa shukrani “Kiukweli kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa Meridianbet ambao wameonesha moyo wa utu kwangu kwa kunipatia msaada, Lakini ningependa kuwaomba msiishie kwangu muweze kuendelea kuwaidia wengine wenye uhitaji”

Leave A Reply