The House of Favourite Newspapers

Meridianbet Yamwaga Ajira Temeke, Zaidi ya Watanzania 142 Wanufaika

0

ZAIDI ya watanzania 142 wamenufaika na ajira kupitia Meridianbet Tanzania, ikiwa ni moja ya ndoto ya kampuni hiyo inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni.

Akizungumza katika uzinduzi wa duka la Meridianbet lililopo Mtaa wa Tandika Majaribio, Temeke, Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu, alisema kuwa kama kampuni, wana malengo madhubuti ya kimkakati ya kutengeneza ajira za moja kwa moja kwa watanzania wengi wenye uhitaji mkubwa kwa sasa na kwa baadaye.

“Hatimaye leo tumezindua duka la Meridianbet hapa Mtaa wa Tandika Majaribio, Wilaya ya Temeke, baada ya uzinduzi wa duka hili, tunatumaini litatoa ajira zaidi kwa ndugu zetu ambao watafanya kazi hapa na maduka yetu mengine zaidi ya 18 yaliyopo maeneo tofauti hapa Tanzania.

“Mpaka sasa Kampuni ya Meridianbet inayotoa huduma za michezo ya kubashiri mtandaoni, imesaidia kutoa ajira kwa zaidi ya watanzania 142 ambao wanafanya kazi kwenye maduka yetu yaliyosambaa nchi nzima, ikiwemo hili la Max 25 hapa Tandika Majaribio,” alisema Nkurlu.

Alisema kuwa lengo kubwa la Meridianbet ni kuhakikisha wanatoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wao, bila kujali jinsia, kabila, rangi wala rika ilimradi tu mteja awe ametimiza miaka 18 na kuendelea ambapo anaruhusiwa kujiunga na kampuni yao ambayo alisisitiza ni mabingwa nambari moja wa michezo ya kubashiri kwa sasa Tanzania.

Aliwashukuru wateja wao kwa kuwawezesha kufika hatua walipo sasa tangu wameanza kutoa huduma za kubashiri michezo mbalimbali kama soka na kasino.

Alizitaja huduma zinazotolewa na kampuni yao kuwa ni Odds bomba na kubwa zaidi kwa kila mechi na ligi zote, machaguo ya kila aina zaidi ya 1000 yanayopatikana kwa kutembelea tovuti yao ya www.meridianbet.co.tz

“Kuna huduma moja inapendwa sana ya KUTURBO mkeka wako unapoona unaelekea kuchanika, hii pia ipo Meridianbet. Sio jambo dogo hili, bali ni hatua kubwa tunayopiga pamoja na wateja wetu,” alisisitiza Nkurlu.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wateja wao, Theresa Michael, alisema kuwa duka hilo litampunguzia gharama za kwenda umbali mrefu kubashiri.

“Duka hili litapunguza usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya kubet. Hiyo nauli niliyokuwa natumia, sasa nitaongezea na kuweka dau kubwa zaidi ili nishinde pesa nyingi,” alisema.

Mteja mwingine, Hassan Juma, alisema: “Napenda huduma nyingi za Meridianbet, ikiwemo ile ya kuturbo kwani inanifanya niokoe dau langu endapo kuna timu inaelekea kuchana mkeka wangu, lakini pia machaguo mengi yananipa uhuru wa kuchagua kipi niweke na kipi niache.”

Nkurlu aliongeza: “Tangu mwaka 2019 tulianza kuzindua maduka taratibu ambayo yanamilikiwa na Meridianbet, tukianza na maduka ya Kariakoo, Manzese, Gongolamboto na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam, na mpaka leo Januari 26, 2023 ambapo ni miaka minne inatimia kwa kuzindua duka hili linalofanya kufikia idadi ya maduka ya Meridianbet kutimia 19.

“Lakini pia hilo pekee halitoshi, Kampuni hii inayojitahidi sana kila siku kufungua fursa kwa kila mtu mwenye lengo la kufanya biashara na sisi, anapata nafasi hiyo, Meridianbet tumeamua kutoa uwakala wa maduka yetu jumla 39 yanayomilikiwa na mawakala wetu ambao nao kwa kushirikiana nasi wamekuwa wakitoa huduma nzuri kwa wateja wetu waliosambaa nchi nzima, na hii inatoa ishara ya namna ambavyo Meridianbet imepiga hatua kubwa kwa ukuaji na kudhihirisha ukongwe wetu.”

Aidha, alisisitiza kuwa lengo kuu la Meridianbet ni kuendelea kuzindua maduka mbalimbali na kutanua wigo mkubwa wa masoko kwa kuwafikia wateja wao kwa urahisi na kutengeneza wepesi wa kutoa huduma bora kwa kila mtu.

“Mbali na maduka haya 19 na maduka 39 ya mawakala, jumla yanakuwa maduka 58. Pia Meridianbet tuna kasino ya mtandaoni inayokupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu zaidi. Michezo kama Aviator, Titan Dice, Roullette na mashine za sloti ni moja ya huduma zinazopatikana,” alisema.

Nkurlu alisema kuwa pia wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kurejesha kwa jamii kidogo wanachokipata kwa kutoa misaada mbalimbali kama walivyofanya kwa wanawake wasiojiweza Kibaha, Chama cha Watu Wenye Ualbino (TAS), Hospital ya Tumbi, kufanya usafi ufukweni maeneo ya Kigamboni kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Fatma Almas Nyangasa.

Aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, wateja wao pamoja na wadau wengine wanaofanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa, wakiwaamini na kuwa nao mpaka leo.

Leave A Reply