Messi Anyakua Ballon D’OR

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amefanikiwa kuweka rekodi nyingine kwenye tuzo za Ballon D’OR kwa kutwaa tuzo yake ya Saba.

 

Nyota huyo amefanikiwa kuwashinda nyota wa Bayern Munich Robert Lewandowski na Kiungo Jorginho wa Chelsea huku mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema akiorodheshwa wa nne katika kinyang’anyiro hicho.

 

Messi aliisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutwaa uchampioni wa Copa America mwaka huu hata hivyo hii haikuwa kigezo pekee kilichomfanya ashinde tuzo hiyo bali takwimu zake kulinganisha na washindani wake kwenye tatu Bora kama zinavyoonekana kwenye picha inayofuata.

Messi ameweka rekodi nyingine baada ya kutwaa tuzo yake ya Saba ya Ballon D’OR
2009: Leo Messi
2010: Leo Messi
2011: Leo Messi
2012: Leo Messi
2015: Leo Messi
2019: Leo Messi
2021: Leo Messi.


706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment