The House of Favourite Newspapers

Messi Ashinda Kesi ya Kutumia Nembo ya Jina Lake

0

LIONEL MESS sasa anaweza kusajili jina lake kama nembo baada kushinda mzozo wa kisheria wa miaka tisa, mahakama ya juu barani Ulaya imeamua.

 

Mahakama ya haki ya Ulaya imetupilia mbali rufaa ya ya kampuni ya  baisikeli ya Massi Uhispania na ofisi ya haki miliki ya muungano wa Ulaya, EUIPO.

 

Mchezaji soka huyo wa Barcelona alitoa ombi la kutaka kutumia jina lake kama nembo ya vazi la michezo mwaka 2011. Lakini Massi alipinga ombi hilo likisema kuwa nembo hizo mbili zinakaribiana na huenda ikaleta mkanganyiko.

 

Mahakama ya Ulaya ya Haki (ECJ) imesema hadhi ya mchezaji nyota huyo itazingatiwa kutathmini ikiwa watu wataweza kutofautisha nembo hizo mbili.

 

Kwa kuzingatia hilo, ilidumisha uamuzi uliotolewa 2018 na mahakama ya pamoja ya EU ikisema mchezaji huyo anajulika vyema na kwamba suala la mchanganyiko haliwezi kutokea.

Massi, ambayo inauza baisikeli na vifaa vyake, ilifanikiwa katika hatua ya kwanza ya kupinga ombi la mshambuliaji huyo wa Barcelona. Lakini ilishindwa baada ya Lionel Messi kuwasilisha rufaa katika mahakama ya Ulaya, ambayo imetoa uamuzi wa sasa.

 

Messi, 33, ambaye anavalia jezi nambari 10, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani kwa mara sita mfululizo pia ni mchezaji kandanda anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes. Inakadiriwa kuwa mchezaji huyo alilipwa jumla ya Dola mil. 12 kufikia 2020 (ambazo ni sawa na Paundi mil. 97).

 

Mnamo mwezi Agosti, mchezaji huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka klabu ya Barcelona.

Leave A Reply