The House of Favourite Newspapers

Messi: Kukaa benchi Azam kumenifunza

0

Ibrahim Mussa,
Dar es Salaam
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano ‘Messi’ amesema kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ameweza kujifunza mambo mengi katika maisha ya soka kitu ambacho hakuwahi kukitarajia.

Messi alijiunga na Azam msimu huu akitokea Simba ambapo tangu atue hapo hajawai kufunga bao lolote lakini ametoa pasi mbili za mabao huku akicheza mechi yake ya pili kwa dakika zote 90 wikiendi iliyopita dhidi ya Mwadui FC ambayo walishinda bao 1-0.
Hata hivyo, mambo yanaonekana kuwa magumu kwake ndani ya Azam kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara tofauti na alivyokuwa Simba.
Akizungumza na Championi Jumatano, Messi alisema kamwe hawezi kujutia kukaa benchi katika kikosi cha timu hiyo kwa kuwa ameweza kujifunza mambo mengi ambayo alikuwa hayafahamu katika soka.
“Unajua katika maisha kuna vitu vingi vinatokea lakini watu wengi hawajui binafsi bado najivunia uvumilivu niliokuwa nao wakati wote nilioanza kuwa hapa, sikuwa napata nafasi ya kucheza kwa asilimia zote lakini sasa naweza kucheza kwa dakika 90 maana Simba nilikuwa na uhakika wa kucheza mechi nyingi.
“Kikubwa kilichonifikisha hapa mpaka kocha kuniamini na kunipa nafasi ya kuanza ni kitendo cha kuwa mvumilivu wakati wote nilipokuwa nakosa nafasi ya kucheza kwa dakika zote na wakati mwingine kutocheza kabisa hilo limekuwa ni funzo kubwa kwenye maisha yangu lakini pia kiwango changu kimeimarika zaidi,” alisema Messi.

Leave A Reply