Metacha Achomolewa Yanga, Mshery Atajwa

MABOSI wa Yanga wameliondoa jina la kipa wa zamani wa timu hiyo, ambaye hivi sasa anakipiga Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Bara, Metacha Mnata.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae za Metacha kurejea Yanga katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.

 

Yanga iliachana na kipa huyo katika msimu uliopita kwa kile kilichoelezwa utovu wa nidhamu wakati akikipiga hapo Jangwani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa uongozi upo katika mipango ya kumsajili kipa kwenye dirisha dogo lakini siyo Metacha.

 

Bumbuli alisema kuwa wapo baadhi ya makipa wanaojadiliwa na uongozi, hivyo mara baada ya kukamilika kwa mipango hiyo ya usajili wote, basi watamtambulisha Desemba 31, mwaka huu.

“Wapo makipa wengi tulio katika mipango nao, lakini siyo Metacha ambaye hayupo katika mipango yetu kabisa katika dirisha dogo.

 

“Tunafahamu kuna mipango mingi inafanyika ya kumtengenezea mazingira mazuri Metacha kwa ajili ya kuja kuichezea Yanga,” alisema Bumbuli na kuongeza:

“Kipa Mshery (Aboutwalib) wa Mtibwa yeye siwezi kuzungumzia hilo, lakini upo uwezekano kusajiliwa au kutosajiliwa.”

 

Gazeti hili linaamini kuwa, Yanga imeshamalizana na Mshery ambaye wamempa mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment