The House of Favourite Newspapers

Mexico yaadhimisha mwaka 1 tangu wanafunzi 43 kutoweka

0

Maelfu ya watu wakiwa kwenye maandamano kuishinikiza serikali kutoa ukweli kuhusu vifo vya wanafunzi 43.

Mwaka mmoja uliopita, wanafunzi 43 walipotea katika mji wa Iguala katika jimbo la Guerrero, kusini mwa Mexican.
Maelfu ya watu wanashiriki katika maandamano makubwa katika mji mkuu wa Mexico kuadhimisho mwaka mmoja tangu kutoweka kwa wanafunzi hao.

Maandamano yakiendelea.

Uchunguzi wa serikali ulidai kuwa, wanafunzi hao walikabidhiwa kwa genge moja la uhalifu, ambao waliwauwa na kisha kuteketezwa mabaki ya maiti yao katika eneo la urushwaji taka.

Ripoti hiyo haijakataliwa tu na jamaa ya wanafunzi hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi moja la wataalamu wa uchunguzi huru, hivi majuzi ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.

Bernardo Santos Campos, babake Hose Angel, Ameiambia BBC kuwa wazazi wa wanafunzi hao waliotoweka hawatasitisha maandamano kamwe, hadi watakapojua kilichofanyika.Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.

Kesi hiyo ni nembo ya kutoweka kwa maelfu ya raia wa Mexico, ambao wametoweka katika muongo mmoja wa ghasia inayohusisha makundi hasimu ya ulanguzi wa dawa za kulevya na walinda usalama.

(Chanzo: BBC)

Leave A Reply