Mexime Apokea Changamoto Mbeya City, Kuikoa Kutoshuka Daraja

Baada ya mwanzo mgumu wa msimu, Mbeya City wamemkabidhi timu kocha Mecky Mexime huku jukumu lake kuu likiwa kuhakikisha klabu inabaki Ligi Kuu msimu ujao wa 2026/27.
Hadi sasa, Mbeya City imecheza mechi 10 na kudumu na alama 8 pekee, ikiwa nafasi ya 12 kati ya timu 16 kwenye jedwali la ligi. Hali hii inaonyesha changamoto kubwa kwa timu hiyo, huku kocha Mexime akitakiwa kuongeza kiwango cha wachezaji na kuhakikisha matokeo chanya yanapatawa haraka.
Kocha Mexime sasa anapewa jukumu la kuhakikisha timu inapata alama za kutosha katika mechi zinazofuata ili kuepuka kushuka daraja, jambo ambalo linafanya msimu huu kuwa wa changamoto kubwa kwa Mbeya City.


