The House of Favourite Newspapers

Meya Iringa Aliyevuliwa Cheo Akabidhi Ofisi

0

ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe leo Jumanne, Machi 31, 2020, amekabidhi ofisi pamoja na gari alilokuwa akitumia kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Himid Njovu, baada ya kukamilisha taratibu za kiofisi.

 

Kimbe aliondolewa madarakani kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za halmashauri hiyo katika shughuli binafsi.

 

“Baada ya kupata muhtasari nikafikiria kwamba hata nikisema niendelee kubaki madarakani kitakachofanyika maana yake mkurugenzi hataitisha vikao kwa hiyo nimeona ni busara kuwahurumia wananchi wa Iringa na nikabidhi ofisi ili niruhusu vikao vya halmashauri kufanyika,” amesema.

Leave A Reply