The House of Favourite Newspapers

Meya wa jiji la Dar es Salaam Ziarani Nchini Iran

1
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

NA DENIS MTIMA

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, ameondoka nchini kuelekea Iran kwa mwaliko wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mkutano wa siku mbili utakaofanyika katika Mji wa Bashar.
Mwita akiwa nchini Iran, atapata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran, Hassan Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika Jiji la Bashar utakaohusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.
Baada ya mkutano huo, Mwita ataelekea jijini Tehran kwa mwaliko maalumu wa meya wa jiji hilo, Muhammed Bakir Galbaf ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara na changamoto mbalimbali katika majiji hayo.

Aidha katika mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye majiji ya Dar es Salaam na Tehran.
“ Iran na Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi wamekuwa wakishirikiana na sisi, hii ni fursa pia kwa majiji haya mawili kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi na wao wanataka maendeleo,“ alisema Mwita.
Aliongeza kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais, meya wa Jiji la Tehran ni mmoja wapo.

1 Comment
  1. […] mbalimbali za kijamii. Risasi Vibes, lilikutana naye ndani ya Ukumbi wa Paparazzi, Slipway jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na bendi yake na kufanya naye mahojiano […]

Leave A Reply