MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta leo ametia saini mkataba na Kampuni ya CRJE ya China, inayotarajia kujenga kiwanda cha kuchakata mbolea itokanayo na takataka.
Akizungumza katika hafla hiyo, Benjamin Sitta alisema kwamba ametia saini mikataba kuashiria kuanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mbolea itokanayo na taka ili kuwezesha ukuaji wa viwanda na wakati huohuo kupunguza taka zinazoweza kuzagaa mitaani.