Meya wa Kinondoni na Kinamama wa Sweet Tanzania Spice Walivyochangia Damu

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Dar Songoro Mnyonge ameungana na kinamama wa wajasiriamali wa kikundi cha Sweet Tanzania Spice kuuanga mwezi Machi ambao ulikuwa na siku ya wanawake duniani kwa kujitolea damu kwa ajili ya wahitaji mbalimbali.

Hafla hiyo ilifanyika ofisi za Sido zilizopo Mwananyamala, Dar na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali walioongozwa na Meya Songoro.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mwenyekiti wa kikundi hicho, Halima Koja amesema kikundi hicho ambao kinashughulika na uzalishaji wa majani tiba ambayo ni Melisa Tea, Red Tea pamoja na viungo vingine vya kwenye chai.

Halima amesema wameona wafanye hafla hiyo ya uchangiaji damu baada ya kuona uhitaji mkubwa wa damu hapa nchini kwenye hospitali mbalimbali na kwingineko.
Naye Meya wa Manispaa ya Kionondoni, Songoro Mnyonge amewapongeza kinamama hao kwa kuamua kuuaga mwezi wa siku ya wanawake duniani kwa kuamua kujitolea damu ili ikawa wasaidie wahitaji.

“Hafla nyingi nilizokaribishwa kwenye siku ya wanawake zilikuwa ni za kucheza muziki, kula na kunywa lakini kinamama wa Sweet Tanzania Spice wameonesha utofauti mkubwa kwa kujitolea damu, hivyo nachukua nafasi kuwapongeza damu.
“Nami kwa kuwaunga mkono naungana nao kwa kujitolea damu na kuwaasa watu wengine zikiwemo taasisi na mashirika ya umma kuiga mfano wa kinamama hawa wajasiriamali” alimaliza kusema Meya Songoro.

