The House of Favourite Newspapers

Meya wa Ubungo aishangaa +255 Global Radio

Meya wa Ubungo, Mstahiki Boniface Jacob (katikati) alipokuwa katika studio za +255 Global Radio.  Kulia ni mhariri wa gazeti la Ijumaa, Sifael Paul.

MEYA wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob,  jana  ametembelea kituo cha radio ya mtandaoni ya +255 GLOBAL RADIO na kukiri kwamba inafanya kazi katika kiwango cha hali ya juu.

…Akiwa ndani ya  studio za +255 Global Radio tayari kwa kufanya mahojiano.

Mstahiki Jacob ameyasema hayo alipotembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori katika kuadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alizungumza na kutembezwa katika idara mbalimbali zikiwa ni pamoja na kitengo cha uzalishaji Magazeti Pendwa, magazeti ya Championi na Sport Xtra, Global TV Online, na kitengo cha Teknolojia na Mawasiliano (IT).

Mahojiano yakiendelea ndani ya +255 Global Radio.

Baada ya kutembezwa sehemu hizo, alikiri kwamba alikuwa amevutiwa na utendaji na studio za redio hiyo ambapo alisema “inaweza kuwa namba moja”.

…Akiongozwa na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul,  katika  ofisi za Global Group.
…Akisaliiana na Mhariri wa Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.
…Akiwasalimia wafanyakazi wa +255 Global Radio.
…Akiwa na Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kushoto) na Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula.
…Akimpa ‘Hai’ Sweetbert Lukonge wa Magazeti ya Championi na Sport Xtra.
…Akijuliana hali na Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Hamida Hassan.

Comments are closed.