The House of Favourite Newspapers

Mfahamu K-Lyinn Kabla ya Kuwa Jacqueline Mengi

JACQUELINE NTUYABALIWE  (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 Desemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania.

 

Aliwahi kuwa mwanamuziki, na sasa ni mfanyabiashara ambapo aliwahi kushinda taji la malkia wa urembo nchini (Miss Tanzania 2000). Ni mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo ya Amorette Ltd.

 

Baba yake alikuwa mwenyeji wa mkoani Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mama yake akiwa nesi.

 

Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya Nyakahoja jijini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya sekondari ya Forodhani.

Jacqueline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike ambaye alipendelea sana kusoma vitabu tangu utotoni.

Muziki

Alianza sanaa ya muziki mwaka  1997 akishirikiana na bendi ya The Tanzanites.

Aliimba kama mmoja wa waimbaji viongozi katika kundi hilo kwa miaka mitatu.

Mnamo mwaka 2004 alitoa kibao chake ‘Nalia kwa Furaha’.

Mwaka 2007 alitoa albam nyingine ya ‘Crazy over You’ ambayo ilikuwa kibao cha kwanza cha albam yake mpya iliyoanza kumpa umaarufu.

Alijifunza kuimba kupitia albam za waimbaji  Mariah Carey na Whitney Houston.

 

Malkia wa urembo

2000 Alichaguliwa malkia wa urembo nchini Tanzania baada ya kushinda taji la malkia wa urembo la Miss Ilala ambapo alilitumikia taji hilo kwa mwaka mmoja akizishughulikia jamii mbalimbali.

Katika shindano la dunia la urembo lililofanyika nchini Uingereza , alikutana na watu tofauti waliokuwa na malengo tofauti ambapo anadai kujifunza mambo mengi tofauti.

Tuzo alizoshinda

2007:  Mwanamuziki bora wa kike  Tanzania na kolabo bora kupitia wimbo wake Crazy over you

2007: Mwanamuziki bora kutoka Pearl Music Award

2008: Mwanamuziki bora wa Tanzania

2008: Mwanamuziki bora wa kike Tanzania kutoka Pearl Music Awards

2013: Mwanamke mwenye mitindo bora katika tuzo za fesheni za Swahili

2017: Medali ya shaba ya kimatifa ya Sayari amp,

2017: Medali ya shaba katika orodha ya samani ya Ngorongoro settee,

 

Ndoa

Mwaka 2015 alifunga ndoa na Reginald Abraham Mengi, ambapo wamejaliwa watoto wawili wavulana.

Marehemu mumewe alikuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.

Comments are closed.