The House of Favourite Newspapers

Mfahamu Kazuyoshi… Umri wa Miaka 54 na Bado Anasakata Kabumbu

0

ANAKUAMBIWA umri sio tatizo kwake, huyu ni Kazuyoshi Miura raia wa Japan mwenye umri wa miaka 54, amesaini kandarasi ya kuitumikia Timu ya Suzuka Point Getters ambayo inashiriki ligi ya daraja la nne huko Japan.

Kazuyoshi ambaye alizaliwa February 26, 1967 alianza Kucheza soka la kulipwa mwaka 1986 na ana umri wa soka miaka mitatu zaidi ya Klabu ya PSG ya Ujerumani.

Kazuyoshi aliwahi kuichezea pia timu ya taifa ya Japan kuanzia 1990 mpaka mwaka 2000, alifanikiwa kucheza michezo 89 na kufunga mabao 55.

Amewahi kuchezea timu za Yokohama FC, Tokyo Verdy, Vissel Kob, Kyoto Sanga, Genoa CFC, Sydney FC  kwa nyakati tofauti.

Mafanikio binafsi, Mchezaji Bora wa Mwaka wa Japan mara mbili, Mfungaji Bora wa Mwaka mara tatu, Kombe la Bara la Asia mara moja, Ubingwa wa Ligi ya Croatia mara moja, Ubingwa wa Ligi ya Jappan mara moja na sasa bado yupo sana dimbani.

Umri sio tatizo, neno moja kwa Kazuyoshi👍.

Leave A Reply