Mfanyabiashara Arusha Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 2

MFANYABIASHARA wa jijini Arusha, Kamaljit Hanspaul (58),  ametiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili ama kulipa faini ya shilingi milioni 30.

 

Hanspaul ambaye alishiriki kwa asilimia 100, ujenzi wa nyumba 31 za polisi zilizokuwa zimeungua kwa moto jijini Arusha, alitiwa hatiani kwa makosa matatu ya kuajiri wafanyakazi watatu kinyume cha sheria.

 

Hata hivyo, Hanspaul amefanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru.

 

Wengine walioshtakiwa naye na kutiwa hatiani ni wafanyakazi wake, Vemula Shiva Kumar, Sathasivan Vinoth na Ralph Leopold Hruscka ambapo kila mmoja alihukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya sh, milioni 10 kila mmoja ambapo walilipa fedha hizo.

Toa comment