The House of Favourite Newspapers

Mfanyabiashara Maarufu Nchini PCK, Aadhimisha Kifo cha Mama Yake kwa Kutoa Msaada kwa Jamii

0
PCK

MFANYABIASHARA maarufu nchini Patrick Christopher (PCK) katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha marehemu mama yake mzazi amerudisha tabasamu kwa wanawake/ akina mama wanaojishughulisha na shughuli ya kugonga kokoto katika eneo la Tegeta Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

 

Katika tukio hilo mtangazaji wa kituo cha Habari cha Global TV na 255 Global Radio Zaliam Adam anayeendesha kipindi cha Mapito alishiriki kama mwakilishi wa PCK huku kina mama hao wakisaidiwa Mchele, Maharage, Sukari, Chumvi pamoja na Pesa taslimu kwa ajili ya kuendesha Maisha yao.

Msaada uliotolewa na PCK kwa kina mama wagonga kokoto

PCK amefanya hivyo ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha marehemu mama yake mzazi aliyefariki Septemba 30, 1996.

Grace Nanyaro, ametoa shukrani kwa PCK kwa niaba ya kina mama wote wanufaika

Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo kupitia mwakilishi wake Zaliam Adam ametoa kiasi cha pesa taslimu, Soda pamoja na biskuti kwa kituo cha Watoto Yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Msaada uliotolewa katika kituo cha watoto Yatima cha CHAKUWAMA

Grace Nanyaro mmoja wa akina mama walionufaika na msaada huo wa PCK ametoa shukrani za dhati kwa mfanyabiashara huyo na kumtakia kila lakheri katika shughuli zake.

 

 

Leave A Reply