Mfanyabiashara wa Kenya Aliyepotea Tanzania, Apatikana Mombasa

MFANYABIASHARA raia wa Kenya, Raphael Ongagi,  aliyedaiwa kupotea tangu wiki iliyopita akiwa Tanzania, amepatikana leo Jumanne, Julai 2, 2019,  jijini Mombasa nchini Kenya akiwa hai. Mkewe, Veronica Kundya amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

 

Veronica ameandika:

“Nipo hapa leo nikiwa na furaha kubwa sana sana kuushuhudia UKUU WA MUNGU 🙏🙏🙏. My Raphael AMEPATIKANA leo Mombasa na yupo salama, sina taarifa ingine zaidi ya hio ila hio pia INATOSHA sana kwangu 🙏🙏🙏 .

“Sina mengi ya kusema zaidi ya KUMSHUKURU MUNGU sana sana kwa kuwa yeye ni Mungu wa miujiza maana ametenda 🙏🙏🙏. Napenda KUWASHUKURU WOTE kwa moyo wangu wote kwa niaba ya familia yangu kwa sala na kujitoa kwenu kwa hali na mali kwenye kipindi hiki kigumu.

 

“Mimi na familia yangu tutaishi kutangaza ukuu wa Mungu 💃💃💃💃💃 Mungu azidi kutubariki sisi sote na familia zetu 🙏🙏🙏

MAPYA Ya Mama KANUMBA “Baba KANUMBA Alikuwa MCHEPUKO Wangu ” | KATA MBUGA 


Loading...

Toa comment