MFANYE MUMEO AWAHI NYUMBANI

SIPENDI na wala sitaki kusikia kwani unamkosesha raha mtoto wa mwenzio, kuku wako mwenyewe kwa nini akushikie manati. Kwa nini uishi na mumeo kama kaka yako? Sipendi na kama unatabia hizi ukome na ukomae. 

 

Haya tuendelee na yetu hasa yaliyonifanya nifungue mdomo wangu. Kuna baadhi ya wanawake wenzangu wananiudhi sana kufikia hatua ya kukosa raha, unamuonea haya mumeo au mpenzio mkiwa ndani full khanga sipendi eeeh! Umesikia mwili wako mkiwa faragha si mali yako bali ya mwenzako.

 

Unauficha una kasoro gani mwenzio anahitaji kuliona umbile lililomvutia likiwa na nguo ameliweka ndani ili alifaidi kwa kuliona live, wewe na mikhanga kutwa kucha hata kujipaka mafuta hujipaki mbele ya mwenzio.

 

Mumeo amekuwa akihangaika kuutazama mwili wako kama wewe siyo wake, hupendi kufanya mapenzi mchana na usiku unazima taa.

 

Kufanya hivyo ni kumnyima haki ya msingi mpenzi wako. Hauko pale kwa ajili ya kuvua nguo za ndani tu, la hasha mwanamke ni pambo la nyumba unatakiwa ujiachie muda ukifika hasa ukijua mwenzio anarudi toka kazini kujiweka kwako kwa kuvaa upande mwepesi wa khanga tabasamu alitoki mdomoni huwa tiba sahihi kwa mihangaiko na maudhi ya kutwa nzima.

 

Napenda kukupeni kisa kimoja kuhusiana na tabia ya baadhi ya wanawake kuificha miili yao, kuna jamaa mmoja alioa binti aliyeumbwa akaumbika lakini binti yule alikuwa anamuogopa mumewe kwa kuona kukaa bila nguo mbele ya mumewe kwake ilikuwa aibu kubwa.

 

Muda wote alikuwa na khanga hakupenda kufanya mapenzi mchana, alipolazimishwa sana alikuwa akifunga madilisha na kuvulia nguo kitandani na mumewe akimaliza alikuwa anawahi khanga.

 

Mtindo ule ulimsumbua sana bwana huyo ambaye alikuwa na hamu ya kuuona mwili wa mkewe ambao Mungu aliamua kufanya utundu wake ukimuangalia utafikiri wa kauchora na kupendelewa na mchoraji.

 

Mzee mzima uzalendo ukamshinda na kuamua kutafuta njia ya kuuona mwili wa mkewe bila yeye kujua. Alianzisha mtindo wa kumvizia wakati wa kuoga kumpiga chabo, kutokana na kupata shida ya kuufaidi mwili wa mkewe jamaa aliamua bora awe anapanda juu ya mti ili aweze kumuona vizuri.

 

Jamaa alifanikiwa kupanda juu ya mtu na kumtazama vyema mkewe aliyekuwa akioga, hakuamini chakula kitamu kama kile hukilia gizani.

 

Kutokana na kiwewe alijisahau kushikilia mti na kuporomoka toka juu ya mti mpaka chini. Watu walimshangaa kumpiga chabo mkewe mtu anayelala naye kitanda kimoja. Jamaa alijitetea kwa kusema ukweli kuwa amekuwa akipata shida kuuona mwili wa mpenzi wake, kutokana na tabia yake ya kuuficha muda wote. Ilibidi yule mwanamke awekwe chini na kuelezwa ukweli juu ya tabia yake ambayo inaweza kumpeleka kubaya mumewe.

Baada ya yule mwanamke kugundua kosa lake alipojiachia mumewe alichanganyikiwa, kila baada ya kazi aliwahi kurudi nyumbani, mwanakwetu kujiachia kwa sehemu maalum kwa mwandani wako ni tiba ya kumfanya atulie nyumbani. Hata kama unajisikia basi jipitishe mbele na upande wa khanga halafu jifanye umekudondoka kwa bahati mbaya, kabla ya kuidondosha kohoa kidogo lazima ataangalia hapo idondoshe.

 

Usimuangalie jifanye humuoni lazima atakuwa anakuangalia akifahamu humuoni, iokote taratibu huku ukimuachia aisome namba. Nakuapia lazima mzuka utampanda na kutamani kitu. Usimnyime ni haki yake pia nawe yako. Usimtese mwenzio muoneshe kila kilichomfanya akichague na kukuficha ndani. Kwa haya machache tutapunguza kuzurura kwa waume zetu baada ya kazi. Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

Loading...

Toa comment