The House of Favourite Newspapers

Zari Kuolewa Tena Ndoa ya Tatu, Amtambulisha Mume Wake Kibenteni

0
Zari The Boss Lady.
Zari The Boss Lady ; ni mwanamama tajiri Afrika Mashariki na baby mama wa staa mkubwa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye wikiendi iliyopita alikula bata la haja kwenye viunga vya Jiji la Dar na kuacha misonyo kama yote.

 

Hata hivyo, stori kubwa kwenye familia ya Diamond au Mondi; yaani ukweni kwake ni kwamba walipigwa na kitu kizito baada ya Zari kutinga na mwanaume mwenye umri mdogo (kibenteni) akimtambulisha kama mumewe.
Akizungumza na waandishi wa habari, Zari alimtambulisha mwanaume huyo, siyo tu kama mpenzi wake, bali kama mume wake.

 

“Huyu ni mume wangu, ni mume wangu, kesi kwisha!” Zari alisema

Zari alipoulizwa sababu ya mume huyo wake kujitenga mbali naye wakati akizungumza na wanahabari, alibainisha kuwa huwa anamheshimu na hajihusishi kamwe katika shughuli zake za kazi.

“Niko kwenye kazi na mume wangu na haingilii vitu vyangu za kazi, ananiheshimu,” alisema Zari.


Zari ambaye ni raia wa nchini Uganda mwenye maskani yake pale Durban nchini Afrika Kusini alikataa kufichua jina la mpenzi wake huyo wakati alipoombwa kufanya vile, lakini IJUMAA linamjua kuwa ni kutoka mkoani Iringa, ila anaishi nchini Afrika Kusini.

Hatua hiyo ya Zari kumtambulisha mpenzi mpya inajiri baada ya kuachana na mfanyibiashara wa Uganda miezi miwili iliyopita aitwaye GK Choppa.

 

Waja wamegundua kwamba, Zari amevunja mahusiano yake na GK Choppa pale alipofuta picha zao zote kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Mahusiano ya Zari na mfanyibiashara huyo yalizua utata mitandaoni kwani alionekana kuwa mwenye umri mdogo kuliko.

Mama huyo wa watoto watano anadaiwa kupendelea kujitosa kwenye mahusiano na wanaume wenye umri mdogo kuliko yeye.

Zari ni ex wa Diamond ambaye walijaaliwa kupata watoto wawili pamoja, Tiffah Dangote na Prince Nillan.
Zari alikiri kwamba kwamba hata kama Diamond hayuko karibu kila wakati, lakini anasaidia na kuchangia pakubwa katika malezi ya watoto wao.

 

Zari aliwahi kuwa kwenye ndoa na mfanyibiashara wa Uganda, marehemu Ivan Semwanga ambaye alifariki dunia mwaka wa 2017 kisha alidai kufunga ndoa na yule King Bae hivyo kama huyo wa sasa naye amefunga naye au atafunga naye ndoa basi itakuwa ni ndoa yake ya tatu.

KAJALA Ammwagia PESA Saraphina, AKIPAFOMU Wimbo wa UPO NYONYO, Cheki ULIVYOMPAGAWISHA

Leave A Reply