Mfaransa Kuwashtukiza Mbao Taifa

KOCHA wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amesisitiza kwamba wataishukia Mbao FC kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa kwa staili ya tofauti kabisa. Simba yenye pointi 42 imeonekana kuwa kwenye fomu nzuri kwa sasa tofauti na wapinzani wao Mbao ambao wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kwenye mechi za Simba na
Yanga ndani ya Mwanza.

 

Msimu uliopita kwenye Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda bao 1-0 na ikiwa ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-2 na msimu huu Kirumba walitoa sare ya mabao 2-2.

 

“Tutaingia kwa staili yetu wenyewe ya mchezo na tutacheza vizuri, nina imani ushindi upo ingawa Mbao sijabahatika kuwaona,”alisema Lechantre ambaye rekodi zake ni kubwa zaidi kimataifa.

 

Spoti Xtra ambalo lilikuwepo kwenye mazoezi juzi na jana, lilimshuhudia kocha huyo akifundisha mbinu mpya ya ushambuliaji na sasa Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Nicoulas Gyan hawatokuwa wakipiga krosi tena kama ilivyokuwa awali.

 

Majukumu hayo yamerudishwa kwa viungo wa kati, Jonas Mkude, Said Ndemla wakisaidiwa na Shiza Kichuya, ambaye anacheza nyuma ya washambuliaji, John

Loading...

Toa comment