The House of Favourite Newspapers

Mfumakule Aibuka Kidedea Kamati Tekelezaji UVCCM Sengerema

0

 

Baraza kuu la Jumuiya ya umoja wa Vijana wa Chama cha mapindu  CCM mkoa wa Mwanza limefanya uchaguzi na kuwapata wajumbe wa Kamati tekelezaji wa Jumuiya hiyo.
Akisoma matokeo ya uchaguzi huo usiku huu  mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema Patrick Mundeba  amewatangaza  washindi wa kamati  tekelezaji kuwa ni Paul Mfumakule aliyepata  kura 83 ,mbuyi Mpoyo aliyepata kura 76 na Lidia Abery aliyepata kura 59.
Katika uchaguzi huo wapiga kura walikuwa 333 huku wagombe walikuwa watano Sabina Sumuni  kura 57na Matokeo Katamu kura 58 hawakuchagukiwa baada ya kura zao kupungua.
Kwa upande wake Paul Mfumakule amewashukuru wajumbe wa baraza kuu kwa kumuona anafaa kuwa mjumbe wa kamati tekelezaji amesema atawatumikia bila woga ili jumuiya hiyo iweze kusonga mbele.
“Kupata kura hizi mumeniheshimisha nitatumia.nafasi hii kuwatumikia tukishirikina kwa pamoja ,amesema Mfumakule.
Mbuyi Mpoye naye amewashukuru wajumbe kwa kumchagua hivyo na.kuwaomba kumpatia ushirikiano wakati akitekeza majukumu yake.
Wajumbe Kamati tekelezaji ya UVCCM wilaya ya Sengerema wameahidi kushirikiana na Baraza kuu kuhakisha jumuiya hiyo inasonga mbele.
Leave A Reply