Mfungwa Aliyesamehewa na Rais JPM Agoma Kutoka Gerezani, Ajijeruhi

KATIKA Sherehe za kuadhimishi kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka Disemna 9, jana Rais Dkt Magufuli alitangaza msamaha kwa jumla ya wafungwa 5,533, ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo ambapo kila mwaka wafungwa huachiliwa.

 

Licha ya kuwa wengi huamini kwamba mfungwa anapopata taarifa kwamba anaanchiwa huru atakuwa mwenye furaha na kuchangamkia fursa hiyo, lakini kiuhalisi hali huwa haiko hivyo kwa kila mtu.

 

Katika hali ya kushangaza Merad Abraham ambaye ni miongoni mwa wafungwa 70 waliosamehewa na Rais Dkt John Magufuli jana Disemba 9, amekataa kuondoka katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya akidai kuwa hana mahala pa kwenda huku akijijeruhi usoni kwa jiwe kwa nia ya kutaka ahamishiwe katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Meradi ambaye alifungwa kwa kesi ya kubaka alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Juni 20, 2000 na alitakiwa kumaliza kifungo Juni 20, mwakani. Kwa sasa mfungwa huyo amepelekwa kwenye zahanati ya gerezani kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hali kama hii hutokea pale ambapo mfungwa anakuwa tayari ameshazoea maisha ya gerezani, na kwamba anaona akitoka nje ya gereza, sehemu ambapo atahitajika kutafuta fedha, mavazi, makazi, ili aweze kuishi atateseka sana, hivyo anaona ni heri kubaki gerezani ambapo hahitaji vitu hivyo vyote kuweza kuishi.

 

Katika hatua nyingine, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Ruvuma, Richard Nyivwe ametangaza kuwa kati ya wafungwa 181 waliotakiwa kutolewa leo mmoja wao amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

 

Licha ya taarifa hiyo, wafungwa wengine waliotoka kwa msamaha wa Rais mkoani Ruvuma wameonesha furaha yao waliomshirikisha pia Mkoa wa mkoa huo, Christina Mndeme katika Gereza la mahabusu Songea.

 

LIVE: MWILI wa BILIONEA MUFURUKI UKIAGWA MUDA HUU DSM
Toa comment