WABUNGE wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu na Zainab Vullu wamechangia magodoro 20 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro uliopo shule ya sekondari Maneromango. Aidha Subira ametoa tanki la maji la lita 2,000 litakalosaidia kuhifadhi maji katika shule hiyo na tanki jingine shule ya sekondari Kolesa iliyopo kata ya Vikumburu.
Wakikabidhi msaada wa magodoro na matanki hayo ya kuhifadhi maji, walisema, msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya Tokomeza Zero iliyoanzishwa hivi karibuni na mkuu wa wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo. “Tumejichanga kila mmoja magodoro kumi, kumi na kwa upande wa maji,mimi nipo karibu na shule ya Maneromango hivyo nimewataka wachote maji kwangu buree “alisema Zainab.
Alieleza, wanafunzi wa kike wanahitaji zaidi maji hivyo kwa hakika kwa misaada hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa. Zainab ,aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia katika tokomeza zero, ili kufikia malengo ya kiwilaya kuinua taaluma. Nae Subira alisema ,wazazi na walezi waelekeze nguvu zao kushirikiana na viongozi na serikali kusimamia watoto kuongeza ufaulu.
“Fuatilieni watoto, kufuatilia maendeleo ya kimasomo kwa wanafunzi wetu, tusiachie walimu, tusijisahu wajibu wetu,”:Mkoa na wilaya imejikita kuinua sekta ya viwanda, kama hatutoelimisha watoto jitihada hizo zitakuwa kazi bure “alifafanua Subira.
Subira alimpongeza Jokate kwa kufanya vizuri kwa kampeni hiyo kubwa.
Awali Jokate alibainisha, tangu kuanza kwa kampeni ya Tokomeza Zero, tayari wamejenga madarasa kumi na bweni moja kata ya Kurui kwa zaidi ya sh. mil. 100.
NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE .
Comments are closed.