‘Mganda’ aimwagia sifa Global TV Online
Shaibu Rashidi ‘Nigga One’.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Shaibu Rashidi ‘Nigga One’, anayefanya shughuli zake za muziki nchini Uganda ametua Bongo na kuifagilia Global TV Online akisema inafanya kazi kubwa hadi nchi za nje inasifika.
Akipiga stori na mwandishi wetu katika ofisi za Global, Nigga One alisema ameona fahari sana kufika ofisi za Global na anatarajia kupiga shoo ya nguvu ya uzinduzi wa albamu yake katika ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem ambao unaomilikiwa na Global.
“Kule Uganda natamba sana na vibao vyangu vya Okoa Maisha, Setingi ya Maisha, Tuombe, Lula ya Maisha na Amaela ambao ndio nimekuja kuutambulisha hapa Bongo” alisema msanii huyo.
PICHA NA ISSA MNALLY/GPL