Mganga Mkuu wa Serikali Atenguliwa, Dk. Grace Magembe Achukua nafasi yake

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Prof Tumaini Joseph Nagu aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka na Sharifa Nyanga, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dk. Grace Elias Magembe kuchukua nafasi ya Mganga Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Magembe alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.